
Jua Haki Zako
27 episodes
Kenya : Uhuru wa wanahabari si mjadala
Rueben Kigame na harakati zake kupigia haki
Unyanyasaji na kunyimwa haki kwa wanawake katika biashara za kimataifa
Kenya : Mchango wa masharika ya kiraia kwa jamii
Katika makala haya tunajikita kuangazia mchango wa mashariki yasiokuwa ya kiserikali kwenye jamii zetu. Tunaliangazia shirika la Corps Africa ambalo kwa ushirikiano jamii mbali mbali nchini Kenya limeendelea kuleta mageuzi kwa raia. Ili jamii kuendelea na kujitegemea inahitaji watu wa kufanikisha baadhi ya maswala kwa jamii kuja na mbinu ya namna gani ya kuwezesha jamii kujiendeleza. Kutokana na hili ndipo Corps Africa nchini Kenya huwatumia vijana kwa kuwatuma katika jamii mabalimbali, ili kusema na hizo jamii na kutambua namna gani au wanahitaji msaada gani.
Kenya: Pesa za majanga haziwafikii waathiriwa
Katika makala haya tunaangazia ripoti kuhusu ufadhili wa majanga na mabadiliko ya tabianchi katika maeneo kame, iliochapishwa na masharika kadhaa likiwemo lile la Oxfarm. shaba ikilenga taifa la Kenya, Ripoti hii inaonyesha kuwa licha ya maeneo haya kuathirika zaidi na ukame, mafuriko na mabadiliko ya tabianchi, bado fedha nyingi hazifiki moja kwa moja kwa wananchi wanaohitaji msaada huo zaidi. Ripoti hiyo ya Oxafarm inaonyesha kuwa mfumo wa ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi nchini Kenya bado una changamoto nyingi, ikiwemo ukosefu wa uwazi, ushirikishwaji mdogo wa jamii, na utegemezi mkubwa wa fedha kutoka nje masharika ya nje
Kenya : Haki za wafanyibiashara wa soko la Kigomba
Katika makala haya tunaangazia haki za wafanyibiashara katika soko la Gikomba nchini Kenya. Kwa muda wafanyibiashara hao wamekuwa wakizozana na serikali kuhusu kipande cha ardhi cha soko hiyo. Skiza makala haya kufamu mengi zaidi.
Kenya : Haki za watoto wa kurandaranda mitaani
Kila mtotto ana haki kwa mjibu wa katiba za kila nchi na maazio ya kimataifa. Katika makala haya tunaanhazia haki za watoto wa kurandaranda mitaani. Skiza makala haya kufahamu mengi.
EAC : Wanawake wasilia nyuma katika harakati za amani
Kila Machi nane dunia, huadimisha siku ya kimataifa ya wanawake, katika makala haya tunaangazia sababu ambazo zimechangia wanawake kuachwa nyuma katika harakati za kutafuta amani. Skiza makala haya kufahamu mengi.
Haki za wakimbizi wanapokimbilia mataifa ya kigeni
Je ni masaibu gani wanayopitia wakimbizi wakati wanapokimbia nchi zao? Skiza makala haya kufahamu mengi.
Kenya: Mchakato wa kutoa taarifa za rushwa kwa tume ya EACC
Nchini Kenya tume ya kupambana na rushwa EACC imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha mali ya umma haiporwi. Ila ni mchakato upi mtu anastahili kufuata kutoa taarifa kwa tume. Benson Wakoli alikiti chini Kipsang Sambae afisa wa EACC, tawi la Nakuru kufahamu mchakato wa kutoa taarifa kwa EACC.
Haki ya kuhifadhi taarifa za Siri
Je unafahamu kuhusu haki ya taarifa zako za siri kuhifadhiwa? na je unatambua hatua unazostahili kufuata iwapo zitatolewa? .
Human Right Watch : Haki zinakandamizwa pembe ya Africa
Makala haya yanaangazia ripoti ya Human Rights Watch iliyochapishwa tarehe 4 Februari 2026, inayozungumzia hali ya kutisha ya haki za binadamu katika eneo la Pembe ya Africa. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa raia wa Sudan, Sudan Kusini na Ethiopia ndio wanaobeba mzigo mkubwa wa vita vya silaha vinavyoendeshwa kwa ukatili, ambapo pande zinazopigana mara nyingi hulenga raia kimakusudi. Human Rights Watch inasema mashambulizi haya dhidi ya raia yamekuwa jambo la kawaida, huku wahusika wakikosa kuwajibishwa. Kufahamu mengi skiza makala haya.
Kenya: Hatua za kutafuta haki kwa dhulma za kinadada mtaani Mathare
Kwa miaka mingi Beatrice Karole amekuwa akijitolea kuhamasisha jamii kuhusiana na hatua za kuchukua wakati wanapokabiliana na unyanyasaji wa jinsia. Akiwa na shirika la kinamama la Wanawake Mashinani Initiative katika eneo la Mathare Jijini Nairobi, amefanikiwa kuwaokoa jumla ya wanawake na watoto 30 katika mwaka 2025 ambao anajivunia kuwa licha ya kunyanyaswa, walipata haki yao.
Kenya: Wakulima wadogowadogo washinda kesi ya Sheria ya Mbegu na Mimea dhidi ya KEPHIS
Nchini Kenya, Sheria ya Mbegu na Mimea (The Kenya Seed and Plants Varieties Act), ambayo ilitishia kuwatoza faini na kuwafunga jela wakulima wadogo kwa kugawana mbegu ambazo hazijaidhinishwa, iliamuliwa kuwa kinyume cha katiba. Mahakama ya Kikatiba katika kaunti ya Machakos nchini Kenya ilitoa uamuzi wa kihistoria Novemba 27 2025 kuhusu uhalali wa Sheria ya Mbegu na Aina za Mimea. George Ajowi amekuwa akifuatilia kesi hii na kuandaa taarifa ifuatayo.
EAC : Dhuluma za kijinsia bado ni changamato kote duniani
Makala haya yanaangazia namana gani dhuluma za kijinsia zinaweza kabiliwa. skiza kufahamu mengi zaidi.
Kenya : Biashara ya ngono miongoni mwa vijana ni donda sugu
Juhudi za pamoja zinaendelezwa ili kukomesha biashara haramu ya wototo pwani ya Kenya. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
Kenya : Ahadi ya serikali kwa jamii za wachache
Kila disemba 18 dunia huadimisha siku ya Kimataifa ya Jamii za Walio Wachache siku inayolenga kuzikumbusha serikali na jamii wajibu wa kulinda haki, heshima na ushirikishi wa makundi ambayo kwa miaka mingi yamekuwa yakidai kuachwa nje mipango ya serikali Nchini Kenya, jamii za walio wachache, zikiwemo jamii za wafugaji wanaohamahama, zimekuwa zikidai hazitambuliwi kikamilifu, kukosa huduma za msingi, na kutengwa katika maamuzi muhimu ya kitaifa. Makala haya yanaangazia mipango ya serikali ya Kenya kwa jamii hizo.
Mpango wa kidijitali uliokwama unavyowanyima wanafunzi elimu ya kisasa Kenya
Mwaka 2016, Serikali ya Kenya ilizindua Mpango wa Mafunzo kwa Njia ya Kidijitali (DLP), ikiahidi kubadilisha elimu ya msingi ya umma kupitia teknolojia. Awamu ya kwanza ikigharimu walipa kodi zaidi ya Shilingi bilioni 30, huku kukiwa na mpango wa kupanua mradi huo kwa makadirio ya Shilingi bilioni 64. Takribani miaka kumi baadaye, mpango huo unazidi kukabiliwa na matatizo makubwa na hatimaye kukwama hivyo kuwanyima wanafunzi wa shule za msingi haki zao za kupata elimu ya kidijitali.Sikiliza
Kenya : Haki ya wafanyakazi nje ya nchi
Katika Juhudi za raia wa Africa Kutafuta ajira nje ya nchi wengine wamejipata katika njia panda. Lakini ubalozi wa Austria nchini Kenya, unasisitiza taifa hilo ni salama kwa wafanyakazi wa kigeni. Skiza makala haya.
EAC : Haki ya matumizi ya mitandao
Je unafahamu haki zako wakati unatumia mitandao? na Je unafahamu kwamba haustahili kuvuka kiwango fulani wakati unatumia mitandao? Paul Brain ni mtaalamu wa matumizi ya mitandao anafanunua masharti ya matumizi ya mitandao.
Kenya: Msimamo wa wavuvi wa Lamu kuhusu mbinu za kuvua samaki
Kwa muda sasa wavuvi kutoka kaunti ya Lamu, nchini Kenya, wamekuwa wakizozana na serikali kuhusiana na mbinu za kisasa wa uvuvi kutokana na misimo wa serikali kuwataka watumie technolojia katika uvuvi. Mwaka 2016 serikali ya Kenya ilipitisha sheria ya kuwataka wavuvi kutumia mbinu za kisasa kuendesha shughuli za uvuvi lakini hili limeibua changomoto miongoni mwa wavuvu wanaosisitiza kutumia mbInu za kale kuendesha shughuli za uvuvi kutokana na sababu kadhaa. skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.
Kenya : Ukeketaji bado changamato Africa
Katika maeneo ya wafugaji wa kuhamahama nchini Kenya, mila na desturi bado zinaonekana kupewa kipaumbele kuliko elimu – hali inayowafanya wasichana kuwa katika hatari kubwa ya kukeketwa. Wasichana wengi hukatizwa masomo na kulazimishwa kufuata tamaduni zinazokiuka haki zao, huku ukeketaji ukiendelea kufanywa kwa usiri mkubwa licha ya juhudi za serikali na wadau kutoa elimu na kupiga marufuku tendo hilo. Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa ukeketaji wa wasichana na wanawake wenye umri wa miaka 15 hadi 49 bado ni tatizo linaloripotiwa nchini Kenya. Katika makala haya tunaangazia namna tamaduni hizi zimeendelea kushamiri katika jamii za wafugaji wa kuhama hama na jinsi zinavyomnyima mtoto wa kike haki yake ya kupata elimu na kuishi bila unyanyasaji.
Matumizi ya hadithi kupigania haki
Katika makala haya tunangazia safari ya kutetea haki za binadamu kwa kutumia hadithi sauti moja, uzoefu, na ujasiri wa mtu kusimulia alichopitia. Tasisi ya Moth, imekuwa ikitumia hadithi kama si tu kwa mudhadha wa burudunai bali ni daraja linalounganisha ukweli wa mtu mmoja na uelewa wa dunia nzima. Hadithi nyingi ni za binafsi, lakini hisia zinazozibeba—hofu, matumaini, maumivu au ushindi—ni za ulimwengu mzima. Skiza makala haya kufahamu mengi.
Mila zanakandamiza wanawake nchini Kenya
Mila na tamaduni kutoka jamii mbalimbali nchini Kenya, zimezidi kukandamiza wanawake kutoridhi mali. Pwani ya Kenya, changamoto hiyo pia imeathiri wanawake wajane skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.
DRC : Ukatili wa jinsia wakithiri
Skiza makala haya kufahamu mengi
DRC : Haki za raia wanaoishi na ulemavu Goma, DRC
Katika makala haya shaba yetu inalenga nchini DRC hasa eneo la Mashariki, ambapo tunajadili haki za malemavu eneo hilo. Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mamia ya watu wenye ulemavu wamejikuta wakihangaika kuokoa maisha yao, kipindi hiki vita vikiendelea kusheheni eneo hilo. Miji kama Goma, Rutshuru na Sake imeshuhudia maelfu wakikimbia maakazi yao. Lakini kwa wengi wenye ulemavu, kukimbia si jambo rahisi. Wengine wanatembea kwa magongo, wengine hutumia viti vya magurudumu ambavyo haviwezi kuvuka matope, milima, au mabonde. Skiza makala haya kufahamu mengi